Psalms 110

Bwana Na Mfalme Wake Mteule

Zaburi ya Daudi.

1 a Bwana amwambia Bwana wangu:
“Keti mkono wangu wa kuume,
mpaka nitakapowafanya adui zako
kuwa mahali pa kuweka miguu yako.”

2 b Bwana ataeneza fimbo yako ya utawala yenye nguvu kutoka Sayuni;
utatawala katikati ya adui zako.
3 cAskari wako watajitolea kwa hiari
katika siku yako ya vita.
Ukiwa umevikwa fahari takatifu,
kutoka tumbo la mapambazuko
utapokea umande wa ujana wako.
Au: vijana wako watakujia kama umande.


4 e Bwana ameapa,
naye hatabadilisha mawazo yake:
“Wewe ni kuhani milele,
kwa mfano wa Melkizedeki.”

5 fBwana yuko mkono wako wa kuume,
atawaponda wafalme siku ya ghadhabu yake.
6 gAtawahukumu mataifa, akilundika mizoga
na kuwaponda watawala wa dunia nzima.
7 hAtakunywa maji katika kijito kando ya njia,
Au: Yeye atoaye mtu wa kurithi mwingine atamweka kwenye mamlaka.

kwa hiyo atainua kichwa chake juu.
Copyright information for SwhNEN